Thursday, August 2, 2012

Picha hizi nimeziiba mjengwa blog wadau.... astakalfiluLah.... Ramadhani hii. wizi si mzuri. ahahaaaaa

 Watanzania wanapenda sana kusoma magaze ila uwezo wa kununua hawana. Nakumbuka nikiwa mdogo baba yangu akinituma magazeti asubuhi watu wananisimamisha njiani wanayasoma weeeee mpaka nachelewa kufika nyumbani. Halafu nachapwa mimi, nilikuwa sielewi kwanini jamaa wale hawakuwa wakinunua magazeti yao, sasa nimeelewa.

Mnakumbuka enzi za mwalimuuu? Ikikaribia sikukuu lazima uende ukashonewe suti. Utasikia mama ama baba wanakuambia fulani na fulani, haya nendeni mkaoge tuende kwa fundi. Vile mkipimwapimwa na fundi mnachekacheka mnajua mambo mazuri sikukuuu hii.

No comments:

Post a Comment