hakika mimi watoto wa mitaani wananinyima raha sana. Hawa niliwapiga picha leo asubuhi chini ya ukuta wa shule ya awali ya Upanga mkabala na maktaba ya taifa . muda ambao walitakiwa kuwa shule wao wanacheza kamari...
Hapa ni karibu na hoteli Kilimanjaro, mito hii sijui inaelekea wapi maana mitaa hii hakuna nyumba za watu ni ofisi tu.
Haki ya nani Tanzania hakuna umasikini, khaaa hili 'jigari' nimeliona kwa macho yangu leo mjini.
Nilikutana na hizi zana za kivita zikipelekwa maeneo husika leo kwa ajili ya sherehe ya kuzikaribisha meli tatu za kivita kutoka Japan. Leo asubuhi zilipokelewa na jeshi la wananchi Tanzania... kwa kupigiwa mizinga 21.
Huyu Kondoo nilimkuta maeneo ya kimara leo asubuhi, nadhani anafikiria Eid inakuja atapona?
No comments:
Post a Comment