Monday, April 15, 2013

Kidojembe inatoa pole kwa wadau wa Taarab nchini kwa msiba wa Haji Mohammed.

 Haji Mohamed (mwenye kanzu) akiwa na mwenyekiti wa chama cha mpira pwani Hassan Hasanoo.

 Haji Mohammed enzi za uhai wake akifurahia jambo alipokuwa studio kurikodi nyimbo zake.

Haji Mohammed katikati wakati akiimba bendi ya Gusagusa akiwa na wakurugenzi wa bendi hiyo kulia ni Rashadi na kushoto ni Fonichupa.
Kidojembe inatoa pole kwa wanafamilia ya mwanamuziki nguli wa Taarab nchini ndugu Haji Mohammed (Mzee wa kilicho chema ni chema), kilichotokea leo asubuhi jijini Dar es Salaam.

Haji mohammed ni kielelezo cha Taarab Tanzania bara na visiwani kwani anatoka katika familia yenye historia kuu ya Taarab, kwani upande wa baba yake ndipo palipotoka mwanamke wa kwanza kuimba Taarab Afrika Mashariki Bibi Mtumwa Saad au Siti Bint Saad.

Marehemu mpaka mauti yanamkuta kutokana na maradhi ya sukari alikuwa mkurugenzi wa bendi maarufu ya Taarab, African Melody. Haji atakumbukwa kwa kuimba nyimbo nyingi zilizolipaisha jina lake kama Kilicho Chema ni Chema, wimbo mwingine siujui jina lake ila naujua mstari mmoja unaimba hivi 'Ishara zitazameni nampenda nami anipenda tunapendaaana." Pia aliimba 'Mambo yetu bambam mimi na mwana wa kwetu'.

Taarifa nyingine kuhusiana na maziko zitatolewa baadaye baada ya kuenda mazishini Kariakoo yalipokuwa makazi ya marehemu. Ila zipo taarifa kuwa mwili wake utasafirishwa leo kuelekea Zanzibar kwa maziko.

Sote ni wa Mungu na kwake tutarejea.

No comments:

Post a Comment