Msanii wa kimataifa Mmarekani, Madonna anafanya mkutano na
rais wa Malawi, Joyce Banda kujaribu kusuluhisha mzozo kuhusu kazi ya misaada
ya msanii huyo nchini humo.
Mwezi
Disemba,shirika la misaada linalomilikiwa na Madonna lilitangaza kuwa limejenga
shule kumi nchini Malawi .
Hata
hivyo waziri wa elimu Eunice Kazembe, alisema kuwa Madonna ameweza tu kujenga
madarasa kumi katika shule zilizopo.
Madonna
ameasili watoto wawili, kutoka Malawi ,
na aliahidi kuwarejesha nyumbani kwao baada ya miaka michache.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment