Shrikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
limeteua waamuzi watakaochezesha mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho kati
ya Azam na Barrack Young Controllers II ya Liberia
itakayochezwa Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam .
Mwamuzi wa kati ni Adelaide Ali, mwamuzi
msaidizi namba moja ni Amaldine Soulaimane wakati Ibrahim Mohame atakuwa
mwamuzi msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ansudane
Soulaimane.
Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10.30
jioni atakuwa Abdelhamid Radwan kutoka Misri. Maofisa hao wa mechi hiyo
watafikia kwenye hoteli ya Holiday Inn.
Wakati huo huo, Barrack Young Controllers II
imewasili nchini leo (Aprili 2 mwaka huu) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya
PrecisionAir ikitokea Nairobi , Kenya inapounganisha safari hiyo inayoanzia Monrovia kupitia Accra ,
Ghana .
Timu hiyo iliyofia hoteli ya Sapphire Court itafanya mazoezi leo jioni
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake kwa
ajili ya mechi hiyo huku wapinzani wao Azam wakiendelea kujinoa kwenye uwanja
wao wa Azam Complex.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
Aprili 2, 2013
No comments:
Post a Comment