Tuesday, August 7, 2012

Jamani eennhhh Abrakadabra anayoipigia kelele kaka Mjengwa inahitaji kupatiwa dawa...



Ndugu zangu,

Huyu bwana nilimkuta maeneo ya Ubungo kituo cha daladala, leo asubuhi akiwadanganya Watanzania ambao hawana mwelekeo wa maisha kuhusu Freemason.

Ati alikuwa anaeleza athari za dini hiyo ya kishetani na aina ya alama zinazotumika. Nilipompiga picha hii alikasirika sana na kudai yeye hapigwi picha bure mpaka alipwe. Hilo pekee limeweza kuniamsha akili kuwa watu aina hii hawana lengo la kuwapa watanzania elimu juu ya masonia, bali wanataka kutengeneza pesa kupitia ndugu zetu waliokata tamaa ya maisha.

Ipo haja Serikali ikaingilia kati zoezi hili, ima kwa kulisitisha ama kuwatoza kodi kubwa watu wanaotembea mabarabarani ama katika vituo vya habari kujidai wanaifahamu sana dini hii mpya ya kishetani. Upuuzi huu ukinyamaziwa baada ya miaka michache tutakuwa tunaongeza mambumbumbu katika Taifa letu.

Kaka yangu Maggid Mjengwa, mmiliki wa blogu ya Mjengwa, amekuwa akipiga kelele sana juu ya mambo haya ya kujidai kutoa elimu ya dini hii ya kishetani na kuita mambo hayo abrakadabra. kama mazingaombwe tu ama kiini macho ambapo hakuna ukweli wala hajulikani nani anapinga na nani anatoa elimu.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
7/08/2012
0713 593894, 0752 593894

No comments:

Post a Comment