Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa, akirejesha
fomu za kugombea nafasi ya ujumbe wa UVCCM-NEC Taifa. Mwingine ni katibu
wa UVCCM mkoani Mwanza Elias Mpanda, katika ofisi za CCM mkoa- Jijini Mwanza.
Mstahiki meya aliweka wazi nia yake ya kutaka kuwawakilisha
vema vijana wa kitanzania kwenye UVCCM-NEC na aliwaasa vijana wengine kushiriki
kwenye mchakato huo na huku akisisitza kwamba yuko tayari kufanya kazi kokote
nchini kwa maslahi ya wananchi, vilevile aliwaasa viongozi wote kuwajibika na
kutimiza ahadi zao walizozitoa kwa wananchi na kwa kuweka mbele maslahi
ya taifa na sio yao binafsi.
No comments:
Post a Comment