Monday, August 6, 2012

Taarifa kwa umma...


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                          WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWEPO KWA MGONJWA WA EBOLA, WILAYA YA KARAGWE MKOA WA KAGERA, TANZANIA


Utangulizi
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma, kuhusu tetesi zilizokuwa zimeenea hapa nchini kutoka kwenye vyombo mbali mbali vya habari kuhusu kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola,wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.

Mnamo tarehe 3 Agosti 2012, Wizara ya Afya na Ustawi Wa Jamii ilipokea taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya ya Karagwe ya kuwepo kwa mgonjwa aliyekuwa anahisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola, katika hospitali ya Wilaya ya Nyakahanga. Aidha,taarifa hiyo ilibainisha kuwa mgonjwa huyo alikuwa ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (6|) kutoka katika kijiji cha Nyakatundu wilayani Karagwe. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali, kulegea, kutokwa damu puani, kutapika damu, na kukojoa damu.Maelezo kutoka kwa mama mzazi zilieleza kuwa mtoto huyu alianza kuugua kuanzia tarehe 30 Agosti 2012, ambapo alipatiwa dawa ya Septrin baada ya hospitali binafsi kuonyesha kuwa ana ugonjwa wa“Typhoid”.

Uchunguzi wa awali katika hospitali ya Nyakahanga ulionyesha kuwa mtoto huyu alikuwa anasumbuliwa na uambukizo kwenye haja ndogo (Urinary Tract Infection).Vile vile alifanyiwa uchunguzi wa kimaabara na Vipimo vya malaria, Hepatitis na Typhoid havikuonyesha kuwepo kwa magonjwa haya. Hospitali inaendelea kumpatia matibabu mtoto huyu na imewaweka mgonjwa na mama yake anayemtunza kwenye chumba maalum (Isolatiom room) kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Aidha mnamo tarehe 4 Agosti 2012, timu za wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na timu ya mkoa wa Kagera imeweza kufika na kumfanyia uchunguzi wa kina pamoja na kuchukua sampuli za damu kwa ajili ya uchunguzi zaidi katika maabara ya Taifa ya uchunguzi wa magonjwa na Maabara za nje ya nchi, ili kubaini kama ameathirika na ugonjwa wa Ebola. Timu hiyo ya wataalamu imetoa taarifa kuwa hali ya mgonjwa huyu kwa sasa imeimarika ikiwa pamoja na kutokuwa na homa, kutapika na kukojoa damu kumekoma pia, uchunguzi uliofanywa kwa mama wa mtoto umeonyesha kuwa hana dalili zozote za ugonjwa wa Ebola.Vile vile hakuna taarifa ya mtu mwingine yeyote kwenye familia hiyo au kwenye maeneo ya kijiji hicho au cha jirani kuwa na dalili za ugonjwa huo.


Kufuatia taarifa hii, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Mkoa wa Kagera imechukua hatua zifuatazo;
• Imepeleka timu ya wataalamu mbali mbali kutoka Wizarani na mkoa kwa lengo la kwenda kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huo.
• Imetoa elimu ya Afya kuhusu njia za kuzuia kuenea ugonjwa wa Ebola pamoja na dalili za ugonjwa huu, kwa wananchi na watumishi wa afya katika hospitali ya Nyakahanga
• Kupeleka vifaa kinga katika hospitali ya Nyakahanga pamoja na maeneo ya mipakani
• Kutoa matangazo kwa jamii kwa kutumia vipaaza sauti na kupitia radioni (Radio Karagwe) kuhusu ugonjwa huu. Aidha, vipeperushi pia vimetolewa.


Hitimisho

Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola hapa nchini.Aidha, Wizara ya Afya imejiaanda kikamilifu kukabiliana na ugonjwa huu iwapo utatokea hapa nchini.

Kwa sasa timu za wataalum zipo katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha, kutoa elimu juu ya ugonjwa huu kwa wataalamu na kwa wananchi na vilevile kufuatilia ugonjwa huu sehemu za mipakani.

Wizara inaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa haraka kwenye kituo chochote cha kutolea huduma za afya, mara wanapoona dalili za ugonjwa huu.


Imetolewa na: kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Afya na     Ustawi wa Jamii
Tarehe 6 Agosti, 2012

Asalaam Alaykum Warahmatu llahi Wabarakatu 

Ama Baada ya Salamu naomba Toa Shukran zangu za Dhati  Timu Nzima ya Blog hii ya Jamii Japo Nimechelewa kuwatakia Kheri ya Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani Wadau wote pamoja na Timu yako Naomba Pokea Salamu zangu na Tunamuomba M/Mungu azipokee Funga Zetu na Dua zetu kwa Ujumla.

Naomba Nita barouk kidogo ( Tupate barka )  kwa Pamoja kwa kukumbushana Siku hii Muhimu katika Siku ambazo Ndio zimeufanya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kuwa Mwezi Mtukufu  nayo Ni Siku ya LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO).

LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) NI USIKU AMBAO 

UNAPATIKANA NDANI YA MWEZI HUU MTUKUFU WA 

RAMADHANI NDANI YA KUMI LA MWISHO MTUME (S.A.W) 

LILIPOKUWA LIKIINGIA KUMI LA MWISHO ALIKUWA 

AKIZIDISHA IBADA KWA SANA NA KUWA AMSHA WATU 

WAKE ( ALHAL BAYTI ) KWA AJILI YA KUFANYA IBADA 

ZAIDI KATIKA KUMI HILO.

LAYLATU QADIR SI MWEZI 27 TU ILA WENGI WA 


WANACHUONI WAMEJITAHIDI KUWA HIYO NDIO SIKU YA 

LAYLATUL QADIR

SIKU HII INAPATIKANA NDANI YA  MWEZI 21 , 23 , 25 , 27 , 


29 , NI JUU YETU NDUGU ZANGU KUITAFUTA SIKU HII 

KWA KUFANYA 

IBADA KWA WINGI NDANI YA KUMI LA 

MWISHO ILI M/MUNGU ATUWEZESHE KUIDIRIKI SIKU 
AMBAYO UBORA WAKE NI ZAIDI YA MIEZI 1000 NA 
HUSHUKA MALAIKA NDANI YA SIKU HIYO KWA IDHINI YA 
M/MUNGU SUBHANAHU WATAALAAH .

UTUFUKU WA SIKU HII NI UNAPATIKANA KWA MAMBO 
MAKUU MAWILI KUTEREMKA KWA QUR AN ( MUNGOZO 
WA MUISLAM)

KUSHUKA KWA MALAIKA KWA IDHINI YA MOLA MTUKUFU.

NA IBADA YA SIKU HII UBORA WAKE NI ZAIDI YA MIEZI 
1000.

 NI JUU YETU KUHAMASISHANA NAKUKUMBUSHANA 
KUWA SIKU HII SI SIKU MOJA NA MUHIMU SANA ILI 
KUPATA KUMUOMBA MUNGU NA KULIOMBEA TAIFA LETU 
NCHI YETU YA TANZANIA MUNGU KULIPA BARKA.

SIKU HII MUNGU AKIKUBARIKI KUIDIRIKI DUA YA 
KUOMBA 
NI HII KWA MAELEKEZO YA MAMA AISHA 
alimuliza Mtume 
Jee? tukiidiriki LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) tufanye 
nini ? Mtume akajibu kithrisha kusema NASH-HADU ANLAA 
ILAAHA ILLA ALLAHU NASTAGHFIRULLAH NAS'ALUKAL 
JANNATA ILAAHI WANAUDHUBIKA MINA NNAAR 
ALLAHUMA INNAKA AFUWUN TUHIBUL AFWAA 
FA'AFUANNAA YAA KARIYMAL AFWU ". Kama alivyosema Mtume

MUNGU NDIYE MJUZI WA HII SIKU LAKINI INAPATIKANA 
NDANI YA KUMI LA MWISHO LA RAMADHANI.



Ghalib N Monero.
Al- Azhar University 
Cairo Misri

No comments:

Post a Comment