Waziri wa Mambo ya nje
wa Marekani Bi Hillary Clinton amezitaka Sudan
na Sudan Kusini kumaliza
uhasama baina yao .
Akizungumza mjini Juba amesema uhasama ambayo ulizifanya nchi hizo mbili
zikaribie vita hazifai kwa nchi ambazo ni jirani.
Bi Clinton ndiye afisa wa kwanza wa ngazi ya juu
zaidi wa Marekani kuzuru nchi hiyo tangu ijipatie uhuru Julai mwaka jana.
Makataa
iliyowekwa na Umoja wa Mataifa ya kutaka nchi hizo mbili kumalizi tofauti zao
kuhusu malipo ya upitishaji wa mafuta ilikamilika jana.
Sudan
Kusini ndio nchi ya pili ambayo Bi Clinton anazuru katika ziara yake ya mataifa
saba ya bara Afrika.
Waziri
huyo aliwasili Juba majira ya alasiri akipitia Senegal
akitokea ,Uganda .
"Ijapo
Sudan na Sudan Kusini sasa
ni nchi tofauti lakini maendeleo yao yanategemea
uhusiano kati yao ,"
alisema baada ya kukutana na Rais Salva Kiir was Sudan Kusini.
"Ni
jambo la dharura kwa nchi hizi mbili, Kaskazini na Kusini, kuendelea
kujadiliana ili muafaka kuhusu utata baina yao uweze kupatikana.
"Kila
moja ya nchi hizo ni sharti zilegeze misimamo yao
iliklupunguza uhasama kati yao "
Matamshi
ya Bi Clinton akiwa Senegal
yaliolaumu sera za serikali ya China
kuhusu sera zake barani afrika matamshi yake yameshutumiwa na vyombo vya
serikali ya China .
Katika
taarifa yake mjini Dakar Bi Clinton alisema Marekani inazingatia zaidi mfumo wa
uhusiao wenye manufaa kulko ule wa kunyonya raslmali.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment