Takriban watu kumi na
moja wa kabila la Pokomo wameuawa katika mashambulizi mapya ya kulipiza kisasi
katika eneo la Tana River,Kusini Mashariki mwa Kenya .
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alisema alisikia
watu wakipiga mayowe wakati kijiji kimoja kilipokuwa kinashambuliwa na kisha
wenyeji kuteketezwa.
Eneo hilo
ambako zinaishi jamii za kuhamahama ni kitovu cha mizozo ya ardhi na maji kati
ya jamii za Orma na Pokomo.
Watu
wengine kumi walijeruhiwa kwenye uvamizi huo uliotokea usiku wa kuamkia leo.
Uvamizi
huu umetokea baada ya mashambulizi mengine kutokea mwezi jana ambapo watu 52
kutoka jamii ya Orma wengi wakiwa watoto na wanawake kuuawa kwa kunyongwa na
kuteketezwa kiasi cha kutotambulika.
Ni
katika tukio ambalo lilitajwa kuwa ghasia mbaya za kikabila kutokea katika
miaka ya hivi karibuni nchini Kenya .
Polisi na viongozi wa kijamii walisaidia kutuliza hali na kurejesha usalama
kati ya jamii hizo mbili lakini hali ya wasiwasi iimeendelea kutanda.
Licha
ya kwamba polisi waliahidi kuimarisha hali ya usalama katika eneo hilo , viongozi wa eneo hilo wanasema vikosi vya usalama vimeshindwa
kuzuia ghasia.
Mbunge
wa eneo hilo ,
Danson Mungatana amewashtumu maafisa wa usalama kwa kushindwa kuchukua hatua za
kuwalinda wananchi licha ya kufahamu mapema kwamba mashambulio yatatokea.
Jamii
hizo mbili za Pokomo na Orma, zimekuwa zikizozana kuhusu matumizi ya ardhi na
maji ambazo ni rasilimali adimu.
Wapokomo
ni wakulima ambao hukuza chakula kando ya mto Tana wakati jamii ya Orma wakiwa
wafugaji wa kuhamahama.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment