Saturday, April 13, 2013

Jana wakati napita maeneo ya jengo la Sayansi na Teknolojia niliona maajabu.

 Jua lilikuwa kali lakini maji yamejaa na kusababishia usumbufu watembea kwa miguu, magari tu ndiyo yalipita.
                                Pikipiki zilipita lakini kwa taaabu sana, tazama jamaa anavyoelea.

 Hapa kawaida kunajaa madereva Tax, wauza chakula na wauza magazeti lakini siku ya jana kama unavyoona.

 Huu ni upande wa pili wa jengo sehemu kunapoengeshwa magari ya maji taka, yaani jengo zima lilikuwa limezungukwa na maji tena yanalwenda kwa kasi ya ajabu utadhani mvua kubwa inanyesha kumbe jua kali.


Hii ni chemba ya mai taka inafurika maji balaa sasa sijui ndiyo chanzo cha balaa lote hili ama kuna mahala kwingine....

HAFIDH KIDO
kidojembe@gmail.com
12 april, 2013
Dar es Salaam, Tanzania.

No comments:

Post a Comment