Friday, April 12, 2013

Picha za jana katika tamasha la taaluma Kigoda cha Mwalimu Nkrumah Hall.

 Mgeni Rasmi siku ya jana jaji mkuu wa mahakama Kenya Dk Willy Mutunga akisalimiana na wadau.

 Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, akisalimiana na wazee wenzie majaji na wanasiasa wastaafu katika ukumbi wa Nkrumah. Wa kwanz akushoto ni mwalimu mstaafu Mama Getrude Mongela.

 Mzee Joseph Butiku msaidizi wa hayati Mwalimu Nyerere akisalimiana na Dk Mutunga jana.

 Majaji wastaafu wakipiga soga ndani ya ukumbi wa Nkrumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya tamasha kuanza. Wa kwanz akushoto ni Jaji mstaavu Lubuva ambae ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.

 Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam wakiwa wamepanga mstari ili kupata kitabu cha "Miongozo miwili, kupaa na kutunguliwa kwa Azimio la Arusha' Kilichotungwa na Prof Issa Shivji Nyagoda anaemaliza muda wake na msomi mahiri Mwalimu Bashiru Ally.

 Mzee Kingunge akibadilishana mawazo na wazee wenzie ndani ya ukumbi wa Nkrumah jana.

 Jaji Mutunga akizungumza na jaji mstaafu Mihayo, makamu mkuu wa chuo Prof Rwekaza mukandala, pamoja na Nyagoda Prof Issa Shivji kabla ya kuanza tamasha jana.

 Kingunge akitambulishwa Dk Mutunga na Nyagoda prof Issa Shivji jana.

 Mwenyekiti wa gazeti la Raia Mwema Jenerali Ulimwengu akighani shairi wakati wa ufunguzi jana.


 Dk mutunga akizindua kitabu cha "Miongozo Miwili, Kupaa na kutunguliwa kwa Aizimio la Arusha"

 Wanafunzi kutoka Kenya wanaosoma katika chuo kikuu cha Dar es Salaam wakiongozana na Dk Mutunga katika viunga vya chuo kikuu hicho.

Jembe jana nilikutana na rafiki yangu Seif Abalhasan ambae ni msomi na mwanamajumui mkubwa. Ninaiba sana kazi zake katika ukurasa wake wa facebook.

HAFIDH KIDO
kidojembe@gmail.com
12 April, 2013
Dar es Salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment