Thursday, April 11, 2013

Leo nimeamua kuwawekea picha za kigoda cha mwalimu, ila kesho ambayo ni siku ya mwisho nitaandika makala nzuri kuhusu mdahalo huu wa umajumui wa Afrika.

 Profesa Issa Shivji ambae ndie mwenyekiti wa kigoda cha taaluma cha Mwalimu Nyerere akimkaribisha mgeni wa siku ya leo Profesa Anna Tibaijuka.

Profesa Shivji akimsindikixa Profesa Tibaijuka kupata chai, huku mvua ikinyesha baada ya mdahalo wa asubuhi kuisha.


 Huu ni msimu wa kigoda, chuo kizima cha Dar es Salaam kimepambwa kwa maneno yanayoashiria sherehe hizo.

 Kingunge Ngombare Mwiru akizungumza na mmoja wa maprofesa waalikwa katika ukumbi wa Nkrumah leo.

 Jembe nikipata chai asubuhi katika eneo la Mdigiree, chuo kikuu cha Dar es Salaam.

 Profesa Samir  Amin, ambae ameandika kitabu cha 'long road to Socialism' ambae mwaka jana alikuwa mgeni mashuhuri katika sherehe hizi, nae alikuwepo mwaka huu. Profesa Amin anatoka Misri na ni muumini wa siasa za ujamaa hasa akipendelea mawazo ya Karl Max.

 Profesa Anna Tibaijuka akichezea simu yake akiwaonyesha vijana yeye si mgeni wa teknolojia.

 profesa Amin akitoa mada yake kuhusu chakula na ardhi katika bara la Afrika.

 Profesa wa uchumi Ibrahim Lipumba akiwasilisha mada yake kuhusiana na tatizo la chakula duniani, hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania.

 Profesa Shivji akibadilishana mawazo na mmoja wa wadau wa kigoda cha mwalimu leo, kwenye ukumbi wa Nkrumah.

 Wanafunzi wakinunua vitabu na majarida ya wasomi wa ki Afrika nje ya ukumbi wa Nkrumah.





 Mgeni rasmi katika mada ya leo Profesa Jayash Gosh akiwa na mwenyeji wake ambae ndie aliekuwa akiongoza mada leo Profesa Wangwe ndani ya ukumbi wa Nkrumah.


No comments:

Post a Comment