Wanawe rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela,
wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi wake watatu kutoka katika
makampuni anayoyamiliki.
Hii ni kwa mujibu wa vyombo ya habari nchini humo.
Makaziwe na Zenani Mandela wanadai kuwa watatu
hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani
ya dola milioni 1.1
Mmoja
wa wasaidizi hao, ambaye pia ni wakili wa Mandela, George Bizos,amekana madai
hayo.
Kesi
hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa
miaka 94
Mandela
aliondoka hospitalini baada ya kutibiwa ugonjwa wa mapafu pamoja na homa ya
mapafu.
Mandela
alilazwa hospitalini mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili.
Duru
zinasema kuwa kumekuwa na mzozo wa kichinichini tangu mwaka 2005 wa kudhibiti
pesa zinazotokana na mauzo kwenye jina la Mandela hususan picha alizokuwa
anachora akiwa jela.
Makaziwe
na Zenani Mandela waliwasilisha kesi mahakamani wakidai kuwa bwana Bizo, waziri
wa nyumba, bwana Tokyo Sexwale na wakili wa zamani wa Mandela, Bally Chuene,
hawakuwahi kuteuliwa kama wamiliki au wakurugenzi wa kampuni ya Harmonieux
Investment Holdings na Magnifique Investment Holdings, kulingana na gazeti la
Star.
Pesa
zinazotokana na makampuni hayo zinapaswa kuwafaidi wanawe Mandela na yeye
mwenyewe.
"Bizos,
Chuene na Sexwale hawakuwahi kuteuliwa rasmi kama
washika dau katika kampuni hiyo.''
Bwana
Bizos, wakili anayeheshimika sana na ambaye pia
ni rafiki wa karibu sana
wa bwana Mandela, alisema kuwa watajitetea vikali katika kesi hiyo.
Aliongeza
kuwa wanawe Mandela walikuwa wanataka kuuza vitu ambavyo havipaswi kuuzwa .
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment