KAMATI ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imempiga faini ya Sh. 200,000 kila mmoja na kufungiwa mechi tatu wachezaji Joseph Mapalala, Yohana Mirobo, Noel Makunja, Mkome Pastory na Rudenzi Kilinga wa Polisi Mara kwa kufanya vitendo vinavyoshiria ushirikina na kumkimbiza mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Morani iliyochezwa Machi 9 mwaka huu.
Adhabu za wachezaji hao ni kwa mujibu wa kifungu cha 27(1)(g) cha Kanuni za FDL.sh. 400,000 na kumfungia mechi sita Kocha wa
Rhino Rangers, Renatus Shija kwa kushiriki vitendo vinavyoashiria imani za
ushirikina na kumdhihaki mwamuzi kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kifungu cha
31(1)(a) na (b) cha Kanuni za FDL ambapo Kocha huyo aliyeipandisha daraja Rhino
Rangers kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) alifanya vitendo hivyo kwenye mechi
mbili tofauti.
Mechi hizo ni kati ya Kanembwa JKT na Rhino
Rangers iliyochezwa Februari 23 mwaka huu Uwanja wa Lake
Tanganyika mjini Kigoma, na ile kati ya Rhino Rangers na Morani
iliyochezwa Machi 17 mwaka huu Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Pia klabu ya Rhino Rangers imepigwa faini ya sh.
200,000 kutokana na Polisi Wanajeshi- MP kuwapiga walinzi milangoni kwenye
mechi hiyo dhidi ya Kanembwa JKT ili kupisha washabiki wa timu hiyo waingie
bure uwanjani.
Mchezaji wa timu ya Pamba ya Mwanza, Leonard
Nahole amepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi nne baada ya kumrushia
chupa ya maji mwamuzi kwa madai amependelea kwenye mechi dhidi ya Polisi Tabora
iliyochezwa Machi 16 mwaka huu.
Aidha Klabu ya Villa Squad imepigwa faini ya sh.
150,000 kwa kuchelewa uwanjani kwenye mechi yake dhidi ya Ashanti United wakati Majimaji imepigwa faini ya
sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi dhidi ya Mbeya City
iliyochezwa Uwanja wa Majimaji.
Vilevile Msimamizi wa Uwanja wa Majimaji
aliyetambulika kwa jina moja la Mapunda aliwatukana waamuzi kwenye mechi hiyo,
na suala lake litafikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya
TFF kwa ajili ya hatua za kinidhamu.
Pia uongozi wa Uwanja wa Mafinga unaotumiwa na
timu ya daraja la kwanza ya Kurugenzi umetakiwa kuufanyia marekebisho,
vinginevyo hautatumika kwa mechi za FDL msimu ujao.
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
Aprili 10, 2013
No comments:
Post a Comment