Saturday, April 6, 2013

Media Day 2013 ilifana sana.....

 Kulwa Karedia mhariri wa gazeti la Mtanzania akiondoa hatari katika lango lake leo viwanja vya Leaders Club.

 Wanahabari wakongwe hawa Mohammed Mharizo kulia na Mahmoud Zubery wakifuatilia michezo katika viwanja vya leaders Club leo wkati wa Media Day, waandishi zaidi ya 1500 walikutana kusherehekea kwa kula, kunywa na kucheza michezo mingi.

 Ahahahaaa Blogers FC wamiliki wa Blogs Tanzania wakipanga list ya soka leo ambapo walikuwa wakishiriki katika tamasha la wanahabari.

 Kidojembe nikiwa na Maggid Mjengwa ambae alikuwa anajiandaa kuingia uwanjani kumenyana na Radio Maria. Maggid ni mmiliki wa Mjengwa blog ambayo sasa imekuwa website.


Mzee Kitime nae alikuwepo, Hapa akiangalia picha aliyopiga kama inaridhisha. Mzee Kitime ni mwanamuziki wa siku nyingi katia Band ya Njenje, lakini nae ameingia katika mambo ya habari blog, hivyo ni mwenzetu.


 Huyu anaitwa Kelvin Kimaro, nilisoma nae shule ya Msingi mjini Tanga. Bombo Primary School, hapa akifurahia Coupon niliyompa akapate bia.

 Mwenyekiti Maggid akiwa mpole baada ya timu yake kuchapwa 3-0 na Radio Maria katika tamasha leo.

 Huyu ni mmiliki wa Handeni Kwetu blog, pia ni mwanahabari gazeti la Mtanzania, anaitwa Kambi Mbwana.

 Mmiliki wa FullShangwe blog, John Bukuku, wa tatu kutoka kushoto mwenye fulana nyekundu akisikitika vijana wake wa blogers fc wakichapwa 3-0 na Radio Maria.

 Mhariri wangu wa gazeti la Raia Mwema Godfrey Dilunga, nae alikuwepo katika tamasha hapa akijifurahisha kwa kucheza volley ball.

 Timu ya IPP Media wakicheza Volley Ball na timu ya TSN, TSN waliovalia blue na nyeupe walitawazwa mabingwa kwa Volley Ball leo.

kocha msaidizi wa Simba SC Jamhuri Kihwelu Julio, akibadilishana mawazo na wanahabari wa michezo leo.

 Jembe nikiwa na wanahabari enzangu niliopata kufanya nao kazi New Habari, wa kwanza kutoka kulia ni Justine Damian anaandikia The African, na wa kati ni Denis Luambano (Mtanzania gazeti), huyu ndie nilianza nae uandishi mwaka 2005. Tumezunguka sana mitaani tukiwa na njaa... dah...


Anaitwa Mpokigwa Mwakapiso au Kigwa one, nilisoma nae TSJ uandishi wa Habari, yeye ni mtangazaji wa Radio Uhuru.


 Ahahahaaa leo nimewaandama wenzangu, hapa timu ya blogers, tulikuwa tunapanga siku ya kukutana. Maana timu ya watu wenye blogs imeanzishwa siku moja kabla ya leo, yaani jana. Hivyo hapo baada ya kuona ni jambo jema kuwa na umoja wa wamiliki wa blogs tumeamua tutakuwa tunakutana kwa mwezi mara moja.

 Wa kwanza kushoto no Makata Mbukuzi na wa tatu kulia ni Ally Kondo, wote ni watangazaji wa Radio Kheir FM, na wote wametoka Radio Saut ya Quran FM. Nimejuana nao kupitia Abbas El Sabry ambae ni baba yangu mdogo ingawa hanifikii kiumri.Nae ni mtangazaji wa Radio Kheir FM na pia alitokea Radio Saut ya Quran, Hivyo sisi watano yaani Makata, Ally Kondo, Abbas na mimi ni marafiki wa miaka mingi sana. Pia walikuwepo Leaders Club.

Kutoka kushoto ni Kambi Mbwana, kati ni Godfrey Nangai niliandika nae pamoja The African, na wa tatu ni Evans Magege anaandikia Mtanzania.

HAFIDH KIDO
6 APRIL, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment