Waziri Samia Suluhu Hassan akipata Maelezo juu ya Ujenzi wa Kituo cha tasisi ya Sayansi za Bahari kilichopo Chukwani Unguja kwa Kaimu Mkurugenzi Dkt Christophet Muhando wakati waziri alipofanya Ziara ya Kutembelea Tasisi za Jamhuri za Muungano wa
Kaimu Mkurugemzi waTaasisi ya Sayansi ya Bahari ya chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt Christopher Muhando akimtembeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Jengo la Taasisi ya Sayansi ya Bahari huko Chukwani Mjini Unguja wakati wa Ziara yakutembelea taasisi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . [PIcha na Ali Meja]
Na Ali Issa Maelezo, Zanzíbar.
ZAIDI ya shilingi bilioni 14 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa chuo
cha Taasisi ya Sayansi za Bahari kilichopo Buyu Wilaya ya Magharibi nje
kidogo ya mji wa Zanzibar.
Hayo yamesemwa leo
huko Forodhani mjini Zanzibar na Muhadhiri Dkt. Ntahondi Nyandwi wakati
alipokuwa akisoma ripoti ya chuo hicho na rasilimali zake mbele ya Waziri anayeshughulikia
masuala ya Muungano Samia Suluhu Hassan aliyekuwa katika mfululizo wa ziara
yake kuzitembelea Taasisi za muungano, Zanzibar.
Amesema fedha hizo
zitahitajika ili kukamilisha ujenzi wa jengo lote na miundombinu
ikiwemo vifaa vya maabara, sehemu za wanafunzi wa shahada za uzamili,
uzamivu, kumbi za mikutano, ofisi za programu za kimataifa, ofisi za
wageni wa kimataifa na mengineyo.
Dk. Nyandwi amesema
kupatikana kwa fedha hizo kutakamilisha mahitaji hayo na mengine ambapo
kwa sasa ujenzi huo umefikia hatua nzuri na wameshatumia zaidi ya
bilioni nne kwa kujenga miundo mbinu mbalimbali ikiwemo ofisi za viongozi
na madarasa.
“Kwa vile pesa za
kumlipa mkandarasi hazikupatikana kwa wakati na hakukuwa na uhakika kuzipata,
ujenzi ulisimama Agosti 2008 na mkandarasi aliondoka lakini kwa sasa ujenzi
unaendeleo taratibu”alisema Nyandwi .
Aidha alifahamisha
kuwa ujenzi huo unaendelea kidogo kidogo kadri fedha zinavyo patikana
baada ya kumuomba mkanda rasi awapunguzie gharama na kuweza kumaliza mipango ya
awamu ya kwanza na ya pili.
Nae Waziri wa
Nchi Afisi ya Makamu wa Rais, Muungano Samia Suluhu Hassan
amesema kuwa atamuagiza Mkuu wake wa kazi kuja Zanzíbar kujionea na
yeye Jengo hilo hatua ilio fikiwa.
Aidha alisema kua
ujenzi huo utaendelea kidogokidogo mpaka utapomalizika.
Maendeleo ya ujenzi
wa Taasisi ya sayansi Baharini ni moja ya Taasisi za Chuo Kikuu cha
Dar-es Salaam kampasi ya Mwalimu Nyerere ambapo umuhimu wa Taasisi hiyo
ulianza kujitokeza Mwaka 1978 chini ya sheria Na. 12 ya 1970 ya chuo kikuu cha
Dar-slamu kwa tamko la Serikali Na. 34 lililo pitishwa tarehe 16 march 1979.
Chuo hicho
kumalizika kwake kufanya kazi za kutafiti nyanja zote za Sayansi za Baharini,
kutoa mafunzo ya uzamivu, uzamili katika sayansi ya Bahari ,kutoa ushauri wa
kitalamu ,kutoa mafunzo ya Shahada ya kwaza kwa kulingsana na mahitaji ya
Taifa la Tanzania kama sehemu ya Taluma kwa vitendo.
IMETOLEWA NA IDARA
YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 5/4/2013
No comments:
Post a Comment