Monday, April 1, 2013

Mgodi uliokuwa na wachimba migodi 14 umeporomoka katika eneo la Moshono , mjini Arusha Tanzania.



Hadi kufikia sasa wakati shughuli za uokozi zikiwa bado zinaendelea, maiti watatu wameweza kuondolewa kutoka kwenye mgodi huo.
Mwandishi habari aliyeshuhudia shughuli hiyo ya uokozi, Ali Shemdoe anasema kuwa pia lori mbili zimefukiwa.
Hii sio ajali ya kwanza ya mgodi kutokea Arusha, nyingine ilitokea miaka saba iliyopita na kusababisha vifo vya watu saba.

Wakati huohuo Rais wa Sudan Omar al Bashir, ameagiza kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa vikao vipya vya bunge, Rais Bashir alitoa wito wa kufanyika mashauriano na vyama vingine vya kisiasa.
Wiki jana makamu wa rais Ali Osman Taha aliwaalika waasi kutoka majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile,kushauriana kuhusu katiba mpya.
Hata hivyo walikataa mwaliko huo.
Waandishi wa habari wanasema kuwa hali ya wasiwasi imeanza kupungua kati ya Sudan na Sudan Kusini tangu nchi hizo mbili zikubaliane kurejelea shughuli ya kuchimba na kusafirisha mafuta.
Chanzo: BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment