Familia ya William Ruto ikiwa katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kukamilisha ziara yao nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Ruto ambaye
alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Akiongea na mgeni
wake katika hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara, Rais Kikwete amempongeza Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya Mhe.
Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya .
Kikwete, pia
alimuelezea Mhe Rutto furaha yake pamoja na kuridhishwa na namna uchaguzi
ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.
Alizungumzia
matumaini yake ya kuwa urafiki uliopo kati ya Tanzania
na Kenya
utadumishwa pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Mhe Rutto, ambaye
aliwasili mkoani Mara wiki iliyopita akiwa na mkewe na watoto, ameondoka jana
jumatatu baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.
CHANZO: IKULU
No comments:
Post a Comment