Monday, April 8, 2013

"MIONGOZO MIWILI, KUPAA NA KUTUNGULIWA KWA AZIMIO LA ARUSHA" ni nini? Soma ndani kuhusu kitabu cha Willy Mutunga jaji mkuu Kenya.
Ujenzi wa Ujamaa si Lelemama bali ni Mapambano, Mapmbano ya Kudumu dhidi ya Upebari na Unyonyaji, dhidi ya Wapinga Maendeleo na Wababaishaji wa Kisiasa, dhidi ya Wahujumu Uchumi, Majambazi, Wezi, Wazururaji na Wazembe.

Msimamo sahihi wa Mapambano unaotokana na Nadharia sahihi ya Ujamaa ungelituepusha na Maamuzi na Vitendo ambavyo vimerahisisha kuoteshwa kwa Mizizi ya Ubepari, kinyume cha Msimamo wa Mapambano dhidi ya Ubepari.

Leo Upebari una vishawishi vingi zaidi Nchini kuliko ulivyokuwa kabla ya Azimio la Arusha kwa sababu pamoja na kwamba sasa tuna sekta kubwa ya umma lakini kutokana na udhaifu wa kutopambana nao, Ubepari umefaulu kujipanua na kujipenyeza hata ndani ya Sekta yenyewe ya Umma.

Na ndiyo maana Ubepari sasa unathubutu kujitokeza hadharani kuukashifu Ujamaa, kubabaisha baadhi ya Viongozi na kututaka tubadilishe siasa zetu.

Ukurasa wa 138 - 139.

Kitabu kimeandaliwa na Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere Juu ya Umajumui wa Afrika cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Maandishi yamekusanywa na Dr. Bashiru Ally, Profesa Saida Yahya- Othman na Mkigoda Issa G. Shivji.

Mchoro wa Gamba la Juu la Kitabu Hiki ni Kazi Njema ya Kipawa cha Msanii na Mchora Vibonjo Mashuhuri Nchini Bwana Ally Masoud Kipanya, Uchapishaji wa Kitabu Ukifadhiliwa na Shirika letu la Haki Elimu.

Kitazinduliwa siku ya Kilele ya Tamasha la Tano la Kitaaluma la Mwalimu Nyerere, Ijumaa ya Tarehe 12 Mwezi wa Nne Mwaka huu na Jaji Mkuu wa Kenya, Dr. Willy Mutunga.

Kitabu Kitatolewa Bure mara baada ya Uzinduzi kwa Wahudhuriaji wote wa Tamasha la Siku tatu ambalo litaanza Jumatano Tarehe 10 kwa Kuzinduliwa na Mada nzito ya Tafakuri ya Miaka 50 ya Uhuru wa Afrika itakayoongozwa na Profesa wa Kigoda wa Mwaka huu ambaye ni Profesa Thandika Mkandawire. Tamasha litaendelea Siku ya Alhamisi na kumalizikia Ijumaa ya Tarehe 12 Mwezi huu katika Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Shime Waungwana Jitokezeni. Tujadili, Tulumbe na Tulimbane.

Mungu Ibaraiki Afrika.
Chanzo: Ukurasa wa facebook, Seif Abalhassan 

No comments:

Post a Comment