Monday, April 8, 2013

Kikao cha matumizi salama ya bioteknolojia chafunguliwa leo jijini...

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava, akifungua Kikao cha wadau kuhusu kanuni za matumizi salama ya Bioteknolojia ya kisasa, kikao kilihusisha wanasanyansi, wanasheria, Mtandao wa wakilishi wa wakulima na Taasisi za Mbegu jijini leo.


 Baadhi ya Wadau wakifuatilia mjadala, katika kikao kazi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu Eng. Ngosi Mwihava (Kulia) akibadilishana mawazo na Dr. Alois Kullaya kutoka Kituo cha Utafiti cha Mikocheni mara baada ya kufungua kikao cha kanuni za Matumizi salama ya Baiotoknolojia ya kisasa.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Eng. Ngosi Mwihava mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi cha wadau kuhusu kanuni za matumizi salama ya Baiotoknolojia ya kisasa kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Makamuwa Rais Mtaa wa Luthuli JijiniDar es Salaam.{Picha na Ali Meja]
No comments:

Post a Comment