Afisa mmoja mkuu nchini Mali
anasema kuwa Mali
inatarajiwa kumpelekea rais wa Ufaransa Ngamia mwingine baada ya yule wa kwanza
waliokuwa wamempa kama zawadi kuchinjwa.
Rais Francois Hollande alimwacha Ngamia huyo na familia moja
kumchungia baada ya kukabidhiwa na wenyeji kama
zawadi mwezi Februari.
Wanajeshi wa Ufaransa walitumwa Mali
mwezi Januari ili kuweza kutwa eneo la Kaskazini kutoka mikononi mwa wapiganaji
wa kiisilamu
Alipompokea
mnyama huyo, Bwana Hollande alisema kwa mzaha kuwa atamtumia kwa safari zake za
jangwani.
Maafisa
wa Ufaransa walikuwa wanapanga kumsafirisha mnyama huyo hadi Ufaransa na
kumweka kwenye hifadhi ya wanyama lakini kwa sababu ya ugumu wa mpangilio wa
safari hiyo, wakaamua kuikabidhi familia moja jukumu la kumchunga mnyama huyo.
Waziri
wa ulinzi, wa Ufaransa alimfahamisha rais kuhusu kuchinjwa kwa Ngamia huyo.
Afisaa
wa Mali
alisema punde waliposikia kuhusu habari hiyo waliweza kumpa rais Ngamia
mwingine ambaye walisema alikuwa na afya nzuri zaidi kuliko yule wa kwanza
aliyekuwa amepewa.
Ngamia
huyo mpya atapelekwa Paris .
“Tumeaibika sana
kwa kile kilichotokea. Ilikuwa zawadi na haikupaswa kufanywa hivyo,” Ilisema ofisi
ya Rais wa Ufaransa.
Ufaransa
ina wanajeshi 4,000 nchini Mali
wakisaidiwa na Maelfu ya wanajeshi wa Mlai , Chad na kutoka nchi zingine za
Afrika.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment