TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA), kimetangaza kuanza kwa Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam, hatua
ya sita bora.
Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, amesema
hayo leo Aprili 5 kuwa ligi hiyo itaanza Aprili 9 mwaka huu hadi 31 katika
viwanja vitatu vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kinesi na Makurumla.
Alizitaja timu zitakazochuana katika hatua hiyo
kuwania kucheza Ligi ya Kanda Taifa kuwa ni pamoja na Boom FC ya Ilala, Friends
Rangers ya Magomeni, Abajalo FC ya Sinza, Red Coast ya Mburahati, Day Break ya
Magomeni na Shariff Star ya Ilala.
“Kwa mujibu wa ratiba yetu, kila siku kutakuwa
na mechi tatu, hivyo katika mechi za ufunguzi Aprili 9, Boom FC wao watachuana
na Shariff Star, kwenye Uwanja wa Airwing, wakati Day Break watamenyana na
Friends Rangers uwanja wa Makurumla huku Red Coast
wao watacheza dhidi ya Abajalo,” alisema Mharizo.
Timu tatu katika ligi hiyo zitawakilisha mkoa
katika Ligi ya Kanda Taifa hapo baadae.
Wakati huo huo, Mharizo amesema kabla ya kaunza
kwa ligi hiyo, kutatolewa semina elekezi kwa viongzi wa timu shiriki,
itakayofanyika Jumapili kwenye Ukumbi wa Shule ya BenjaminMkapa kuanzia saa nne
asubuhi.
“Lengo la semina hii elekezi ni kutoa elimu kwa
viongozi na wachezaji ili kuondoa mvutano wakati wa ligi hiyo, nia yetu ni
nzuri na tunapenda kuona ligi ikichezwa kwa kufuata kanuni na taratibu
zilizowekwa,” alisema Mharizo.
Semina hiyo itawahusisha
Katibu, Mwenyekiti, Kocha, Nahodha na Waamuzi 16 watakaochezesha ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment