Wednesday, September 5, 2012

Kazi imeanza Iringa kuwasusia Polisi...


Hapa wanahabari wakitoka nje ya ukumbi baada ya kususa..Hapa wakiwa wamezagaa, huyu mwanahabari wa mbele mweupe alievalia mabuti ni jembe langu hilo linaitwa abdulfatah Murtadha, niligonga nae nondo TSJ. Amehamia Iringa kikazi.


Wanahabari wa Iringa mchana wa leo wamegoma kupokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa kifo cha Mwandishi Daudi Mwangosi, aliyeuawa juzi jumapili katika mkutano wa ndani wa Chadema uliokuwa ufanyike katika kijiji cha Nyololo Iringa. Mkuu huyo alikataa shariti la wandishi la kumtaka atoe taarifa hiyo bila kuwepo kwa polisi yeyote katika mkutano huo. Kitendo hicho cha mkuu huyo kukataa shariti  la wanahabari kikapelekea waandishi kutoka nje ya ukumbi huo.Hivyo zoezi hilo kushindikana.

Picha zote kwa hisani ya Mjengwa Blog...

No comments:

Post a Comment