Takriban watu 42
wamefariki baada ya basi walimokuwa wakisafiria kuanguka katika Korongo kusini
mwa Morocco .
Zaidi ya abiria wengine
ishirini walipata majeraha mabaya.
Basi hilo
lililokuwa linasafiri kati ya miji ya Marrakesh
na Zagora, lilianguka umbali wa mita 150 kutoka barabarani
Wengi
wa abiria waliokuwa wanasafiri kwenye basi hilo
wanaaminika kuwa raia wa Morocco .
Haijulikani ikiwa kuna majeruhi wowote wa kigeni walikuwa kwenye basi hilo .
Duru
zinaarifu kuwa ajali hiyo ilitokea katika eneo lenye milima mapema leo asubuhi.
Bado
haijulikani kilichosababisha ajali yenyewe ingawa afisaa mmoja mkuu anasema
kuwa uchunguzi umeanzishwa.
Takriban
watu 24 walijeruhiwa , ishirini na moja kati yao
wakikimbizwa hospitalini mjini Marrakesh
na waliosalia wakipelekwa hospitalini mjini Ouarzazate.
Katika
taarifa yake, mfalme wa nchi hiyo Mohammed wa sita, alitoa rambi rambi zake kwa
familia za waathiriwa na kuahidi kulipia usafiri na gharama za mazishi.
Mwezi
Julai mwaka jana, ajali mbili tofauti za basi nchini humo zilisababisha vifo
vya watu 26.
Zaidi
ya watu 4,000 walifariki katika ajali tofauti za barabarani nchini Morocco mwaka
jana kulingana na takwimu za wizara ya usafiri nchini humo.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment