Serikali ya Kenya imesema
kuwa haiwezi kutimiza matakwa ya walimu wa shule za misingi wanaogoma nchini
humo huku mgomo wao ukiingia siku ya pili.
Waziri wa elimu Mutula Kilonzo
ameelezea BBC kuwa matakwa ya walimu ya kuongezwa asilimia miatatu ya mishahara
yao haiwezekani
kwa sababu pesa hizo hazikujuimshwa kwenye makadirio ya bajeti ya mwaka huu.
Waziri huyo aliongeza kuwa walimu hao
walichezewa shere miaka kumi na tano iliyopita wakati walikubaliana na serikali
wakati huo kwamba mishahara yao
ingeweza kuongezwa kwa asilimia miatatu.
Maelfu
ya walimu nchini Kenya
walianza mgomo wao rasmi hapo jana wakidai kuwa serikali imekuwa ikipuuza kilio
chao kuongezwa mishahara kwa miaka mingi.
Walimu
hao ni wa shule za misingi na zile za upili na leo wamesusia kazi wakitaka
nyongeza ya mishahara huku shule nyingi nchini humo zikiathirika.
Walimu
hao wamekiuka agizo la mahakama lililoharamisha mgomo huo. Shule nyingi katika
miji mikubwa mfano Mombasa , Nairobi na Nakuru zilisalia kufungwa.
Walimu
wa shule za upili pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu wamesema watajiunga na
mgomo huo baadaye wiki hii ingawa tayari wameanza kususia kazi.
Mgomo
huu unajiri wakati shule zikifungua kwa muhula wa tatu kitu ambacho walimu hao
wanasema sio hoja kwani wamekuwa wakigoma kila muhula wa tatu unapofungua kwa
zaidi ya miaka kumi iliyopita wakidai hiyo nyongeza.
Wanasema
kuwa serikali haina usawa katika mishahara kwa wafanyakazi wa sekta ya umma
kwani ni hivi maajuzi tu wauguzi na wafanyakazi wengine wa umma walipoongezwa
mishara baada ya kugoma. Wanadai kuwa walimu wamepuuzwa.
Mgomo
huu umeonekana kufanikiwa kwani shule nyingi zimesalia kuwa bila walimu
wanafunzi wengi wakibaki nyumbani.
Walikuwa
wamebeba mabango yenye ujumbe kwa serikali kuwa wao hawawezi kula panya kwa
mishahara midogo ambayo wanapata. Na vile vile walisema kuwa wamechoka na ahadi
za uongo za serikali.
Mgomo
huo uliitishwa na mashirika ya wafanyakazi yanayowakilisha takriban walimu laki
mbili na nusu.
Wameahidi
kuendelea na mgomo hadi matakwa yao
yatakapotimizwa.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment