Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi barabara ya Tanga – Horohoro leo, ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14
akisaidiana na Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto
za Milenia wa Marekani (MCC), Balozi wa Marekani nchini Mhe Alfonso Lenhardt,
Barabara hii ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha
Tanzania na nchi jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata
msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia
(Millennium Challenge Corporation – MCC). Kukamilika kwa barabara hii ni
utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu muhimu
ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua
fursa za kibiashara kati ya Tanzania
na Kenya
na hivyo kutumia vizuri zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti kama
kumbukumbu yaq ufunguzi rasmi barabara ya Tanga – Horohoro ambayo
imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14. Kuhsorto kwake
ni Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia
wa Marekani (MCC), na kulia kwake ni Balozi wa Marekani nchini Mhe
Alfonso Lenhardt.
Msafara
wa Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ukipita juu ya sehemu ya barabara ya Tanga –
Horohoro.
Picha na IKULU.
No comments:
Post a Comment