Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na
Simba iliyochezwa jana (Aprili 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000
kutokana na watazamaji 11,458.
Viingilio katika mechi hiyo namba 155
iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
10,198,220.34.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya
uwanja sh. 7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh.
4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
1,849,326.14.
Wakati huohuo taarifa ya TFF inasema
Watazamaji 11,021 walikata tiketi kushuhudia
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Oljoro JKT iliyochezwa juzi
(Aprili 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam na kuingiza sh. 63,170,000.
Viingilio katika mechi hiyo namba 156
iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 vilikuwa sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
14,853,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
9,636,101.69.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya
uwanja sh. 7,552,501.25, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh.
4,531,500.75, Kamati ya Ligi sh. 4,531,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 2,265,750.37 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
1,762,250.29.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
Aprili
15, 2013
No comments:
Post a Comment