Mechi tano kati ya sita za Super
Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zioneshwe moja kwa moja (live) na
Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini sasa hazitaoneshwa
kutokana na matatizo ya kiufundi.
Kwa mujibu wa
Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport Kanda ya Afrika, Max
Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha mechi hizo kutokana na
matatizo ya kiufundi katika magari
Mechi hizo ni kati
ya Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na Simba, Coastal Union na
JKT Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga itakayochezwa Aprili 17 mwaka huu jijini
Tanga.
Tatizo hilo pia
limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo hazitaonekana wikiendi
hii. SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya televisheni kwa ligi hiyo ya
Kenya.
Tshunungwa amekutana na
Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo hilo. SuperSport kwa
kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga mechi nyingine za Super Week
kabla ya ligi kumalizika msimu huu.
Pia TFF, Kamati ya
Ligi na SuperSport walikuwa na mkutano mfupi wa waandishi wa habari wakati wa
mapumziko kwenye mechi ya leo kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa
Taifa kujadili suala hilo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
13 April, 2013
|
Saturday, April 13, 2013
Matatizo ya kiufundi yakwamisha super week, mechi tano kutooneshwa Live na SuperSport.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment