Margaret Thatcher, alishinda uchaguzi mkuu mara tatu
nchini Uingereza, na kuwa mama wa kwanza kuwahi kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu na
mmoja wa viongozi waliokuwa na ushawishi mkubwa katika karne ya ishirini.
Utawala wake umekuwa na athari kubwa katika sera za warithi
wake wa chama cha Conservertive na pia chama cha Labour.
Bi. Thatcher, ambaye alikuwa na msimamo mkali
kuhusu masuala mbali mbali na wakati mwingine kuchukua maamuzi kutokana na
hisia zake.
Bi
Thather aliongoza Uingereza katika kipindi cha miaka kumi na moja.
Wakati
wa utawala wake maelfu ya raia wa Uingereza walianza kushirikishwa katika
masuala ya kijamii na kiuchumi.
Serikali
yake iliidhinisha sheria ambayo iliwapa raia nafasi kununua nyumba
zilizomilikiwa na baraza la miji.
Serikali
yake pia ilipunguza hisa za serikali katika makampuni kadhaa zikiwemo lile la
kusambaza gesi British Gas na kampuni ya mawasiliano ya simu ya British Telkom
BT.
Lakini
uamuzi wake wa kukataa siasa za makubaliano ulimfanya kuwa kiongozi ambaye
aliwagawanya wengi na wanasiasa wengi walipinga sera zake na mfumo wa serikali
yake hatua iliyopelekea uasi ndani ya chama na maandamano katika barabara za
miji nchini Uingereza.
Ushawishi
wa Babake.
Margaret Hilda Thatcher alizaliwa tarehe 12
mwezi Octoba mwaka wa 1925, katika eneo la Grantham, Lincolnshire .
Baba
yake Alfred Robert na mama yake Beatrice Roberts walikuwa waumini wa dini ya
Kimethodisti.
Babake
alikuwa mmoja wa wahubiri wa kanisa hilo na pia
diwani wa eneo hilo .
Robberts
alikuwa na ushawishi mkubwa maishani mwa mwanawe na hasa sera ambazo
alizitekeleza wakati wa utawala wake.
Bi
Thatcher, alisoma katika chuo kikuu cha Somerville
College , Oxford ,
na kufuzu na shahada ya sayansi na kuwa mama wa tatu kuwahi kuwa rais wa chama
cha Conservative katika chuo kikuu cha Oxford .
Baada
ya kufuzu alihamia eneo la Colchester, ambako aliajiriwa na kampuni moja
inayotengeneza vifaa vya plastiki na alijihusisha na siasa za eneo hilo za chama cha
Conservative.
Mwaka
wa 1949, aliteuliwa na chama hicho kuwania kiti cha ubunge cha Dartford, katika
eneo la Kent
lakini alishindwa katika uchaguzi.
Alipojaribu
tena kuwania kiti hicho miaka na 1950 na 1951 Bi. Thather vile vile alishindwa.
Hata
hivyo kampeini yake iliipa pigo kubwa chama tawala cha Labour, na kama mgombea wa ubunge mchanga zaidi aliangaziwa pakubwa
na vyombo vya habari.
Mwaka
wa 1951, aliolewa na mfanyabiashara Denis Thatcher, na baada ya wakati huo
alirudi chuo kikuu ambako alisomea taaluma ya sheria kabla ya kufuzu mwaka wa
1953, mwaka ambao mapacha wake Mark na Carol walizaliwa.
Mwaka
wa 1955, kwa mara nyingine alijaribu kuwania kiti cha ubunge lakini alishindwa.
Mwaka
wa 1959 akafanikiwa kushinda kiti cha ubunge cha eneo la Finchley.
Baada
ya miaka miwili bungeni, Bi Thather aliteuliwa kuwa naibu waziri na baada ya
chama cha Conservative kushinda uchaguzi wa mwaka wa 1964, aliteuliwa kuwa
waziri.
Wakati
Sir Alec Douglas-Home alijiuzulu kuwa kiongozi wa chama cha Conservative, Bi
Thatcher alimpigia kura Ted Heath, katika uchaguzi wa mwaka 1965 na aliteuliwa
kuwa msemaji wa kamati ya bunge kuhusu masuala ya nyumba na ardhi.
Alifanya
kampeini kali kuhakikisha kuwa wapangaji wa nyumba za mabaraza ya miji
wanaruhusiwa kununua nyumba hizo na alikuwa mkosoaji mkubwa wa sera za chama
cha Labour ambacho kilikuwa kinatoza raia ushuru wa kiwango cha juu.
Wakati Ted Heath, alichaguliwa waziri mkuu
mwaka 1970, aliteuliwa kuwa waziri wa elimu na kupewa jukumu la kupunguza
matumizi ya wizara hiyo.
Moja
ya athari za mpango huo ni kuondolewa kwa zoezi la kutoa maziwa ya bure kwa
watoto wa shule walio na umri kati ya miaka saba na kumi na moja, mpango
uliopingwa na kukosolewa vikali na wanasiasa wa chama cha Labor, huku wengi
wakimwita Bi Thather ''mwizi wa maziwa''.
Akiwa
mmoja wa kina mama wachache katika siasa za Uingereza, kulikuwa na fununu kuwa
huenda siku moja akawa Waziri mkuu.
Madai
kama hayo pia yalienea kuhusu waziri mwingine wa Labour Shirley Williams.
Lakini
kama wanasiasa wengine Bi. Thather alipuuzilia mbali madai hayo.
Katika
mahojiano ya Televisheni Bi. Thather alisema haamini uwezekano wa kuwepo kwa
Waziri Mkuu mwanamke katika maisha yake.
Kutokana
na matatizo mengi, Serikali ya Heath haikudumu kwa muda mrefu.
Baada
ya mzozo uliosababishwa na janga la mafuta mwaka wa 1973, Bwana Heath
alilazimika kuweka sheria ya kufanya kazi kwa siku ili kukabiliana na wachimba
migodi ambao walikuwa wamegoma.
Mwaka
wa 1974, Februari, serikali ya Bwana Health ikasambaratika.
Mama
na mwanasiasa
Bi.
Thatcher, aliteuliwa kuwa waziri kivuli wa mazingira, na kutokana na uamuzi wa
bwana Heath, wa kubadili sera za chama cha Conservertive kuhusu uchumi, Bi.
Thatcher alimpinga kama kiongozi wa chama
hicho katika uchaguzi wa mwaka wa 1975.
Wakati
alipokwenda kwa ofisi ya Bwana Heath kumueleza kuhusu uamuzi huo, Bwana Health,
hakuwa na muda wa kumtazama na kisha akamueleza '' utashindwa''
Na
kinyume ya matarajio ya wengu Bi Thatcher alimshinda Bwana Heath katika
uchaguzi wa chama, hatua iliyopelekea kujiuzulu kwake.
Katika
duru ya pili ya uchaguzi Bi. Thatcher pia alimshinda Willie Whitelaw na kuwa
mwanamke wa kwanza kuwahi kuongoza chama cha kisiasa nchini Uingereza.
Tangu wakati huo, Bi. Thatcher alianza
kuangaziwa pakubwa na vyombo vya habari.
Mwaka
wa sabini na sita, alitoa hotuba kali iliyokashifu sera za serikali ya Muungano
wa Usovieti zilizokandamiza raia wake na wapinzani wa serikali, hatua
iliyopelekea gazeti moja nchini Urusi kumtaja kama
Iron Lady au Mama jasiri, jina ambalo lilimpa furaha nyingi.
Mara
tu alipochaguliwa ushawishi wake ulianza kuwa mkubwa na mwaka wa 1976, alitoa
hotuba ambayo aliyashutumu mataifa yanayowakandamiza raia wake na upinzani.
Huku
akiendelea kuhudumu kama mke na mwanasiasa
anayefahamu uchungu wa kuongezeka kwa gharama ya maisha kwa raia wa kawaida,
Bi. Thatcher alipinga mamlaka ya vyama vya wafanyakazi ambavyo vilikuwa
vikiitisha migomo ya mara kwa mara mwaka wa sabini na tisa.
Wakati
serikali ya Bw. Callaghan ilipoanza kuyumbayumba, chama cha Conservertive
kilichapisha stakabadhi zilizokuwa na kauli mbiu "Labour Isn't
Working" yaani chama cha Labour kimeshindwa.
Jim
Callaghan, alipoteza kura ya kuwa na imani naye tarehe 28 Machi mwaka wa 1979.
Uamuzi
wa Bi Thatcher, wa kuchukua msimamo mkali, ulipokelewa na wapiga kura wengi na
chama chake cha Conservertive kilishinda uchaguzi mkuu.
Sera
za Kiuchumi.
Jukumu
kuu la serikali yake lilikuwa ni kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa muhimu.
Muda
mfupi baada ya kuchukua madaraka alianzisha mpango wa kubuni sera mpya kuhusu
ushuru wa bajeti na pia mpango wa kupunguza matumizi ya serikali.
Miswada kadhaa iliwasilishwa bungeni ya
kupunguza ushawishi wa vyama vya wafanyakazi, kuvibinafsisha viwanda vya
serikali na kuruhusu wapangaji wa mabaraza ya miji kununua nyumba wanazoishi.
Mamilioni
ya watu ambao hawakuwa na jukumu lolote katika uchumi wa Uingereza walijipata
wakiwa na nyumba zao wenyewe na walinunua hisa katika kampuni zilizokuwa
zikimilikiwa na serikali.
Sera
mpya ya kiuchumi iliufanya mji wa London
kuwa moja ya miji inayokuwa kwa kasi na yenye shughuli nyingi na kuwa kituo
kilichofanikiwa kibiashara na kuwa na mfumo wa fedha thabiti duniani.
Kampuni
zilizokuwa zikitumia mifumo ya zamani iliyosababisha uharibifu mkubwa wa
mazingira zilifungwa na kampuni mpya na ya kisiasa zikaanzishwa.
Hali
hii ilisababisha zaidi ya watu milioni tatu kukosa kazi.
Sera
zake zilianza kuwafinya raia badala ya kuleta mageuzi na wabunge wa chama chake
walianzisha vitendo vya uasi.
Baadhi
yao
walimshurutisha kubadilisha sera zake ili kutoa afueni kwa raia na kuokoa chama
hicho kisisambaratike.
Lakini
Bi Thatcer alikataa wito huo, mwaka wa 1980 aliambia mkutano mkuu wa chama
hicho kuwa, wale wanaosubiri kubadili sera zake, watasubiri kwa muda mrefu
zaidi kwa kuwa hana nia wala mpango wa kufanya hivyo.
Vita
vya Falklands
Kufikia
mwaka wa 1981, umaarufu wake ulikuwa umepungua hadi asilimia 25%, kiwango
ambacho ni cha chini zaidi kwa waziri mkuu yeyote.
Hata
hivyo uchumi wa Uingereza ulikuwa umeanza kuonyesha dalili za kuiamarika.
Mwaka
wa 1982, uchumi wa Uingereza uliimarika na umaarufu wake miongoni mwa wapiga
kura ukapanda juu mara nyingine.
Uamuzi
wake pia wa kuidhinisha vita dhidi ya Argentina
kuhusiana na umiliki wa visiwa vya Falkland ,
ulimpa umaarufu mkubwa.
Bi.
Thatcher aliagiza jopo maalum la wakuu wa jeshi kwenda katika kisiwa hicho na
tarehe 14 mwezi Juni wanajeshi wa Argentina walitangaza kuwa
wameshindwa katika vita hivyo.
Ushindi
katika vita hivyo vya Falkland , na mzozo ndani
ya chama cha Labour, kwa wakati huo kikiongozwa na Michael Foot, kiliipa chama
cha Conservertive ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwaka wa 1983.
Mwaka
uliofuatia chama cha wafanyakazi wa migodi waliitisha mgomo wa kitaifa lakini
Margaret Thatcher kwa wakati huu hakutaka kufanya kosa.
Kinyume
na ilivyokuwa wakati wa utawala wa Edward Heath, mwaka wa sabini na tatu,
serikali ya Uingereza ilikuwa imeweka hifadhi ya kutosha ya mkaa katika viwanda
vyake vya kuzalisha umeme, kabla ya mgomo huo kuanza.
Hivyo
mgomo huo haukuwa na athari kubwa kwa shughuli za uzalishaji wa umeme na
kupelekea mgomo huo kumalizika haraka.
Kulikuwa
na makabiliano makali kati waandamanaji na polisi lakini mgomo huo ulimalizika
mwezi Machi mwaka uliofuatia.
Tangu
wakati huo, jamii nyingi zinazotegemea uchimbaji wa madini ya makaa zilishindwa
kujiimarisha kutokana na athari za mzozo huo ambao ulichangia pakubwa
kusamabaratika kwa secta ya uchimbaji wa makaa.
Katika
eneo la Ireland
ya Kaskazini Bi. Thatchet alikabiliwa na mgomo wa kususia chakula kutoka kwa
wafuasi wa chama cha IRA, na msimamo wake mkali kuhusu kundi hilo uliakasirisha
wanasiasa wasiogemea upande wowote na wakosoaji wake wanadai kuwa uamuzi huo
ulichochea waumini wengi wa kanisa la Katoliki nchini Ireland ya Kaskazini
kujihusisha na Ghasia.
Licha
ya kujaribu kuzima uasi uliosababishwa na mzozo huo, kwa kuwapa viongozi wa Ireland , nafasi
ya kuongoza mikakati ya amani, juhudi hizo zilisambaratika kutokana na upinzani
mkali kutoka kwa vyama vya wafanyakazi.
Mwezi
Oktoa mwaka wa 1984, bomu lililotegwa na wafuasi wa IRA lililipuka katika
mkutano wa chama cha Conservertive uliokuwa ukiendelea katika hoteli moja mjini
Brighton .
Watu
watano waliuawa na wengine kujeruhiwa vibaya akiwemo waziri wa serikali Norman
Tebbit.
Na
kama kawaida yake Bi Thatcher, alisisitiza kuwa atachukua hatua kali kujibu
shambulio hilo , wakati wa hotuba yake kwa
wajumbe waliokuwa wakihudhuria mkutano huo, saa chache tu baada ya kutoka kwa
shambulio hilo .
''Shambulio
hilo
limeshindwa. Juhudi zote za kushambulia na kuharibu demokrasia yetu kupitia
vitendo vya kigaidi vitashindwa'' Alisema Bi. Thatcher.
Sera
yake ya nchi za kigeni, ilinuia kujenga hadhi na ushawishi wa Uingereza katika
mataifa ya ng'ambo, jambo ambalo aliamini ilishuka sana chini ya serikali iliyotangulia ya
Labour.
Bi
Thatchter alipata mshirika wa karibu, rais wa Marekani, Ronald Reagan, ambaye alikuwa
na sera za kiuchumi sawa na zake.
Vile
vile alishirikiana kwa karibu na rais wa Urussi Mikhail Gorbachev, ambaye
alikisiwa kuwa rais aliyeleta mabadiliko makuu Urusi.
Chama
cha Labour ambacho kwa wakati huo kilikuwa kikiongozwa na Neil Kinnock,
hakikuwa kimejinusuru kutoka kwa malumbano na mizozo kati ya viongozi na
wabunge wake, hatua iliyompa Bi. Thatcher fursa nzuri ya kushinda awamu ya tatu
kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati wa uchaguzi wa mwaka 1987.
Na
baada ya kuchaguliwa, kitu cha kwanza alichofanya ni kuanzisha ushuru unaotozwa
kwa nyumba na majengo ambao ulikuwa sawa kwa kila mtu ili kugharamia shughuli
za mabaraza ya miji.
Ushuru
huo ulitozwa kulingana na wale wale wanaoishi katika nyumba hizo bila
kuzingatia dhamani ya nyumba au uwezo wao..
Mpango
huo ulisababisha maandamano mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya
Uingereza.
Wabunge
wa chama chake ambao walihofia kupoteza viti vyao, kutokana na ushuru huo,
hawakuwa na njia mbadala ya kufutilia mbali sera hiyo huku Bi Thatcher akiwa
madarakani.
Mwaka
wa 1989 alinusurika jaribio kutoka kwa wabunge wa chama chake la kumuondoa
madarakani, ishara kuwa utawala wake na chama chake ulikuwa umeanza kukabiliwa
na matatizo ya ndani.
Suala
la muungano wa ulaya hatimaye ndio lililosababisha kusambaratika kabisa wa
serikali yake.
Miaka
ya baadaye.
Alipandishwa
cheo na kupewa cheo cha Baroness Thatcher wa kaunti Kesteven katika Kuanti ya Lincolnshire , na alikabithiwa tuzo hilo mwaka 1995.
Aliandika
vitabu viwili kuhusu maisha yake akiwa siasa, kampeini dhidi ya azimio la
Maastricht Treaty na kupinga sera ya serikali ya Serbian ya kuwaangamiza raia
wa nchi hiyo wenye asili ya Bosnia .
Mwaka wa 1997 alimpendekeza William Hague kuwa
kiongozi wa chama cha Conservative lakini alishindwa kumuunga mkono mrithi
wake, Iain Duncan Smith.
Wakati
afya yake ilianza kudhohofika, Bi Thatcher alianza kupunguza shughuli zake za
umma kuanzia mwaka wa 2001.
Baada
ya kukumbwa na mshtuko wa moyo mara kadhaa, madaktari wake walimshauri
kupunguza shsughuli zake za umma na hali yake haijakuwa ya kuridhisha.
Bi
Thatcher pia aliigua ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hali iliyoadhiri pakubwa
uwezo wake kwa mujibu mwa mwanae Carol.
Wakati
mume wake Dennis, ambaye amemtaja kama nguzo
yake kuu, alipoaga dunia mwaka wa 2003 akiwa na umri wa miaka 88, Bi Thatcher
alimlimbikiza sifa chungu nzima.
''
Kuwa Waziri mkuu ni kazi ambayo ina upweke wa hali ya juu. Katika hali moja
hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa kwa kuwa hauwezi kuongoza ukiwa kwenye umati.
Lakini Denis alipokuwa hai sikuwa peke yanagu. Alikuwa mwanamme kamili na mume
na zaidi ya wote alikuwa rafiki wangu mkuu'' Alisema Bi Thatcher.
Mwaka
mmoja baadaye alisafiri nchini Marekani kumuaga mshirika wake wa Karibu
kisiasa, Ronald Reagan katika mazishi yaliyofanyika mjini Washington juni mwaka wa 2004.
Bi
Thatcher aliendelea kujitokeza hadharani, na tukio kubwa zaidi ni uzinduzi wa
sanamu yake mwenyee iliyojengwa katika Bunge la wawakilishi, kitendo ambacho ni
cha kwaza cha iana yake kwa waziri mkuu wa zamani ambaye angali hai akitunukiwa
heshima kama hiyo.
Kwa
mara nyingine alirejea tena katika iliyokuwa ofisi yake iliyoko katika barabara
ya Downing hapa London ,
baada ya Waziri mkuu Gordo Brown kumualika muda mfupi baada ya kuteuliwa kuwa
waziri mkuu.
Mwaka
wa 2010 Bi Thather alirejea tena katika ofisi hiyo akiwa mgeni wa waziri mkuu
David Cameron ambaye alikuwa kiongozi mpya wa serikali ya muungano.
Wanasiasa
wachache sana ambao wamewahi kuwa na ushawishi sawa na wa Bi Thatcher wakati wa
utawala wake na vile vile ni wanasiasa wachache sana ambao wameweza kuwa na
uwezo kama wake.
Kwa wakosoaji wake Bi Thatcher alikuwa
mwanasiasa ambaye aliweka sera ya soko huria kuliko vitu vyote na alikuwa
tayari kuruhusu watu wengine kugharamia sera zake au kuhangaika ili afanikishe
sera zake.
Hii
ilijitokeza sana
kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wasiokuwa na kazi na pia migomo ya
wafanyakazi.
Wafuasi
wake nao wanamsifu kwa kupunguza matumizi ya serikali, kupunguza ushawishi
viongozi wa vyama vya wafanyakazi na kurejesha hadhi ya heshima ya Uingereza
Duniani.
Alikuwa
mwanasiasa ambaye alikuwa na kipaji cha pekee na ambaye alikuwa tayari kutetea
maamuzi yake mazuru au hata mabaya.
Mfumo
wake wa kutokubali kushawishiwa ulikuwa ndio nguzo ya nguvu yake kisiasa na
upungufu wake mkubwa.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment