MECHI ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe
la Shirikisho kati ya Azam ya Tanzania
na Barrack Young Controllers II ya Liberia iliyochezwa jana (Aprili 6
mwaka huu) imeingiza sh. 44,229,000.
Fedha hizo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam
na kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 17,128
waliokata tiketi.
Viingilio vilikuwa sh. 2,000, sh. 5,000, sh.
10,000 na sh. 20,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A.
Kiingilio cha sh. 2,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa
15,212.
Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi
sh. 5,575,500, asilimia 15 ya uwanja sh. 5,798,025, asilimia 10 ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 3,865,350 na asilimia 75
iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh. 28,990,500.
Mechi iliyopita ya raundi ya awali ya mashindano
hayo kati ya Azam na El Nasir ya Sudan Kusini iliyochezwa kwenye uwanja huo huo
Februari 16 mwaka huu iliingiza sh. 34,046,000 kwa viingilio hivyo hivyo huku
ikishuhudiwa na watazamaji 13,431.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment