Mkuu wa polisi wa eneo hilo
Richard Bitonga alisema mwanamume huyo alijitia kitanzi nje ya nyumba yake
katika kituo cha kibiashara cha Lwanda, eneo bunge la Nyatike.
“Alianza kwa kuvaa nguo ya chama cha ODM iliyokuwa na picha ya
Waziri Mkuu kabla ya kujitia kitanzi,” Alisema Bitonga. Ingawa hakuacha
ujumbe wowote, alikuwa amewaeleza marafiki wake kwamba alikasirishwa na uamuzi
wa mahakama.
Baadhi ya wakazi walisema marehemu alikuwa ametisha kujitoa uhai
ikiwa Odinga hangeshinda kesi ya kupinga uchaguzi wa urais. “Alisema hakuona
sababu ya kuendelea kuishi katika ulimwengu huu ikiwa Odinga hatakuwa Rais wa
nchi hii,” alisema mkazi Samuel Otieno, ambaye ni mchimba dhahabu.
Mbunge wa eneo hilo ,
Eric Anyanga alisema “Uamuzi wa mahakama ulishtua wafuasi wengi wa Cord
kote nchini waliotarajia awamu ya pili ya uchaguzi wa urais baada ya dosari
tele kugunduliwa katika uchaguzi wa Machi 4,” alisema Mbunge huyo
Wakati huohuo, Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu wa Rais
Kalonzo Musyoka wanapanga kukutana na maseneta na Wabunge wa Muungano wa CORD
wiki ijayo kujadili hatima yao
ya kisiasa baada ya uchaguzi mkuu kukamilika.
Odinga na Musyoka walikutana na baadhi ya wabunge na
maseneta wa Cord katika ofisi ya waziri mkuu katika barabara ya Harambee Avenue , Nairobi .
Chanzo: Mwananchi.
No comments:
Post a Comment