Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akifafanua
Jambo wakati alipotembelea Mradi wa mpunga kwa njia ya umwagiliaji kwenye
Bonde la Mpunga la Jendele; kulia ni Mwenyekiti wa Tasaf Jendele Ali Mussa.
Mratibu wa wa Programu ya kuimarisha huduma za kilimo Bw Zaki Khamis Juma akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan kuhusu wakulima wa kuzalisha Mbegu za Mpunga kwenye Bonde la Kinyasini -kisongoni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakati wa Ziara ya kutembelea Miradi ya Tasaf na Assp inayofadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akipita kwenye shamba la mpunga la
kuzalishia Mbegu la kinyasini-kisongoni Walaya ya
Kaskazini A Unguja Waziri akiwa katika Ziara ya kutembelea
Miradi iliyofadhiliwa na ASSP [Picha na Ali Meja ]
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu
Hassan amesema kuna umuhimu mkubwa kwa
wananchi kuitunza na kuindeleza miradi inayofadhiliwa na Serikali zote mbili na washirika wa maendeleo ili miradi hiyo
indelee kuwanufaisha wananchi na kutimia lengo lililo kusudiwa.
Hayo ameyasema jana huko Jendele Wilaya ya kati Mkoa wa
Kusini Unguja wakati alipofanya ziara
kutembelea miradi mbali mbali ya kilimo iliyofadhiliwa na TASAF kupitia
Serikali ya muungano Tanzania .
Amesema Serikali imekua ikitoa pesa nyingi kufadhili wananchi
katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa lengo la kuwaweze kujikwamua na
umasikini ili kujipatia kipato.
Amesema wananchi wajifunze kuitunza na kuendeleza miradi
hiyo kwani ina umuhimu mkubwa na kuwanufaisha wenyewe.
“kuiacha miradi ife
si vizuri, muichangie ili iweze kujiendesha na hiyo ndiyo faida ya miradi hiyo”,
alisema Samia.
Aidha Waziri aliwaambia wakulima wa bonde la Jendele Kinyasini
Kisongoni wajitume kwa kuzalisha kwa wingi chakula kwani sasa hakuna sababu kwa
vile maji yapo ya kutosha katika bonde hilo
hivyo uzalishaji ungezeke.
Waziri huyo alisema dhamira ya ziara yake kuja Zanzibar ni kuona vipi matumizi
ya pesa za TASAF zinavyotumika katika miradi iliyoombewa na utekelezaji wake
umefikiaje kwa wananchi.
Waziri alifurahishwa na juhudi zinazochukuliwa kwani
kumefikiwa hatua kubwa za kimaendeleo na zinatia matumaini.
Waziri alitembelea mradi wa
mpunga na mradi wa uzalishaji mbegu za mpunga Kinyasini kisongoni na
badaye kupata maelezo juu ya miradi ASSP na SPDL inayoendeshwa na Wizara ya Kilimo,
Maliasili na Ushirika Zanzibar .
Miradi yaTASAF awamu ya kwaza Zanzibar ilipatiwa dola za kimarekani milioni tatu
ambapo ziligawanywa sawa kwa Unguja na Pemba .
Awamu ya pili TASAF Zanzibar ilipatiwa dola za kimarekani
2,500.000.00 ambapo zilitumika kumalizia
mradi wa kwaza Unguja na Pemba kupitia mifuko mitatu nayo ni mfuko wa Taifa wa
kijiji (NVF) wenye thamani ya fedha TShs 2,500,000,000.00,mfuko wa mradi wa
ukanda wa Bahari (MACEMP) wenye thamani ya fedha TShs 1,800,000.000.00.
Ziara hiyo itaendelea leo kutembelea idara ya uhamiaji Zanzibar na malaka ya
kitambulisha cha Taifa Zanzibar.
HAFIDH KIDO
4 April, 2013
No comments:
Post a Comment