Timu ya Barrack Young Controllers II ya Liberia imewasili nchini leo (Aprili
2 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya
Azam itakayochezwa Jumamosi (Aprili 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam .
Young Controllers imetua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya PrecisionAir
ikitokea Nairobi , Kenya
inapounganisha safari hiyo inayoanzia Monrovia
kupitia Accra , Ghana .
Msafara wa timu hiyo una na watu 37 wakiwemo
wachezaji 21 na ulioongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo Robert
Alvin Sirleaf ambaye ni mtoto wa Rais wa Liberia , Ellen Johnson Sirleaf.
Wachezaji waliomo kwenye kikosi hicho ni Abraham
Andrew, Alfred Hargraves, Alpha Jalloh, Benjamin Gbamy, Cammue Tumamie, Erastu
Wee, Ezekiel Doe, George Dauda, Hilton Varney, Ishmail Paasewe, Joekie Solo,
Joseph Broh, Junior Barshall, Karleo Anderson, Mark Paye, Prince Jetoh, Prince
Kennedy, Randy Dukuly, Raymond Blamonh na Winston Sayou.
Benchi la ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu
Robert Lartey akisaidiwa na Samuel Sumo wakati Meneja wa timu ni Clarence
Murvee. Daktari wa timu ni Samuel Massaquoi.
Timu hiyo inatarajia kundoka kurejea Monrovia,
Aprili 8 mwaka huu kupitia Nairobi, Kenya saa 11.10 alfajiri kwa ndege ya
PrecisionAir.
Chanzo TFF
No comments:
Post a Comment