Hii ni kwa mujibu wa watafiti nchini Japan .
Utafiti huu uliowahusisha watu 37,000,
ulichapisha taarifa kwenye jarida la mtandao, 'BMJ Open' ukisema kuwa wanaume
wanaokuwa na upara kwa asilimia 32 wanaweza kuwa na maradhi ya moyo.
Hata
hivyo, watatifi walisisitiza kuwa athari hizi ni chache ikilinganishwa na zile
za uvutaji sigara na unene kupita kiasi.
Shirika
linalojikita katika maswala ya maradhi ya moyo nchini Uingereza, limesema kuwa
wanaume wanapswa kujichunga wasinenepe kupita kiasi kuliko kuchunga nywele zao.
Kuanza
kukuwa na kipara ni kawaida ya maisha kwa wanaume . Wengi kuanza kukuwa na
upara wanapokuwa miaka 50 na asilimia 80 ya wanaume hao, hupoteza nywele
wanapokuwa na umri wa miaka 70.
Watafiti
katika chuo kikuu cha Tokyo ,
walidurusu utafiti wa miaka mingi iliyopita, kuchunguza uhusiano uliopo kati ya
kuwa na upara na maradhi ya moyo.
Walionyesha
kuwa nywele ambazo zilianza kutoweka, zina uhusiano na maradhi ya moyo. Hii
ilikuwa baada ya kuzingatia maswala kama umri,
na historia ya familia.
Daktari,
Tomohide Yamada , wa
chuo kikuu cha Tokyo
alisema kuwa walipata uhusiano mkubwa kati ya upara na tisho la kupata maradhi
ya moyo.
"tuliona
hili kama jambo muhimu, lakini halina athari kubwa kama mambo mengine
yanayosababisha maradhi ya moyo kama vile
uvutaji sigara, unene kupita kiasi na mafuta mengi mwilini pamoja na shinikizo
la damu.''
Alisema
kuwa wanaume wenye umri mdogo wanaopata upara wanapaswa kuanza kuzingatia afya
njema ili kujikinga kutokana na maradhi ya moyo
Aidha
alisema hakuna ushahidi wa kutosha kupendekeza kuwa wanaume wenye upara
wafanyiwe uchunguzi wa maradhi ya moyo.
Maradhi
ya moyo ndio moja ya sababu kuu za vifo nchini Uingereza.
Mmoja
kati yawanawake wanane kufariki kutokana na maradhi ya moyo.
Husababishwa
na mishipa ya damu ambayo husukuma damu kwa moyo pale inapoziba.
Mmoja
wa madaktari wakuu Uingereza amesema kuwa ingawa utafiti huu unaibua hisia,
wanaume wenye upara hawapaswi kuwa na hofu.
BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment