Desmond Tutu mtetezi haki za wanyonge
Tutu mwenye miaka 87 ametaja Tuzo hii kama
ushindi kwa wote wanaotetea haki za wanyonge bila kubagua.
Askofu Tutu atapokea tuzo hiyo mwezi ujao
mjini London ,
Uingereza.
Akijibu
ushindi huo mwanaharakati huyo wa haki za binadamu amesema kwamba jamii
huwatuza wote wanaotetea haki yao .
Tuzo
hii ilianzishwa mwaka wa 1972 kutolewa kwa raia ambao huchangia zaidi masuala
ya imani na dini bila ubaguzi, ambaye pia hutetea haki za wanyonge.
Mwasisi
wa tuzo hii Sir John Templeton alikua raia wa Marekani lakini akahamia
Uingereza ambapo pia alituzwa na Malkia kwa mchango wake kwa jamii mwaka 1987.
Alifariki
dunia mwaka 2008.Mwaka jana Tuzo ya Templeton ilitolewa kwa Kiongozi wa Kiroho
wa Tibet
Dalai Lama.
Mwaka
jana Askofu Tutu alipokea dola Milioni moja kutoka kwa Wakfu wa Mo' Ibrahim
ambayo hutoa tuzo kwa raia waafrika ambao hutetea haki na ukweli na kutetea
utawala bora.
Desmond
Tutu alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1984 kutokana na harakati zake
dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment